Page 43 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 43
10. Kudhibiti Itikadi za
Kidini na za Kijamii
Mlango 19. Matumaini ya Ivoni
Mlango 20. Dhehebu la Ajabu
Kusikiliza na kuzungumza
Tashbihi za tabia
1. Mwenye bidii kama mchwa au nyuki
2. Mtundu kama tumbili
3. Mzembe kama kupe au chaza au kozi
4. Mjinga kama samaki
5. Mjanja kama sungura au Abunuasi
6. Mkali kama simbabuka
7. Mwoga kama kunguru
8. Mnafiki kama panya au ndumakuwili
9. Mwenye maneno mengi kama chiriku
10. Mnyamavu kama kaburi au mava
11. Wazi kama mchana
12. Mwenye huzuni kama mfiwa
13. Tulia kama maji mtungini
14. Furahi kama mama aliyepata mtoto salama
15. Hasira kama za mkizi
16. Mpole kama kondoo
17. Kuwa n wasiwasi kama kuku mgeni au mwasi
18. Mwenye inda au uchoyo kama joka la mdimu
19. Kuiga kama kasuku
20. Mwenye maringo kama tausi
21. Tumainia kama tai
22. Mvumilivu kama mtumwa
23. Mlafi kama fisi
24. Mwaminifu kama njiwa