Page 42 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 42
Mara kwa mara, magonjwa husababisha migogoro
katika jamii. Baadhi ya wagonjwa kwa mfano, wanaougua
msongo wa mawazo, wasiposhughulikiwa vyema huweza
kuzua fujo.
Magonjwa mengine husababisha watu na mataifa
yawe maskini. Mfano mzuri ni ugonjwa wa Virusi vya
Korona. Kuanzia mwishoni mwa 2019, ugonjwa huu
ulienea haraka katika sehemu nyingi za dunia. Safari
nyingi za ndege, treni, magari na meli zilisimamishwa.
Michezo na mikutano mingi pia ilisimamishwa. Biashara
nyingi pia zilifungwa. Huu ni ugonjwa ulioletea watu
wengi umaskini mkubwa.
Jambo la kuhuzunisha zaidi ni kuwa, mara kwa mara,
magonjwa husababisha vifo. Hii huonyesha wazi kuwa
magonjwa ni adui mkubwa. Tunafaa tujikinge dhidi
ya magonjwa. Yanapotokea, tunafaa kuyashughulikia
ifaavyo.