Page 41 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 41
vyetu vidogo maji na kuelekea kiamboni.
Jioni baada ya kula kilalio, niliamua kumweleza
shangazi mawazo yangu. Nilimwambia kuhusu hatari
ya vyakula na vitafunio alivyozoea kutuletea. Vilevile,
nilimwambia kuhusu hatari za kufulia nguo mtoni.
Shangazi Rukia alinisikiliza kwa makini. Baadaye,
alinishukuru kwa ushauri wangu.
“Huenda ndiyo sababu mimi na watoto wangu, mara
nyingi, huugua. Mara, mafua, mara kukohoa na mara
kuhara na kutapika,” shangazi aliniambia.
Nilipowatembelea tena likizo iliyofuata, mambo
yalikuwa tofauti. Shangazi aliniambia kuwa matatizo yao
ya kiafya yalikuwa yameisha. Hata majirani zao walikuwa
wameacha mazoea ya kufulia nguo mtoni.
Matini 2
Madhara ya magonjwa
Magonjwa ni adui mkubwa wa maendeleo. Magonjwa
husababisha pesa nyingi kutumika katika gharama za
matibabu. Isitoshe, mgonjwa hushindwa kutekeleza
majukumu yake vizuri. Hali hii huleta umaskini. Kwa
mfano, mfanyakazi akiwa mgonjwa, hawezi kufanya kazi
zake ipasavyo. Vivyo hivyo, mwanafunzi akiwa mgonjwa,
hataweza kuyamudu masomo ifaavyo. Ukweli ni kuwa,
umaskini una maafa mengi katika jamii.