Page 47 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 47
Matini 3
Mwashi hodari
Miaka minne baada ya kumaliza masomo ya shule ya
upili, Siero alijiunga na chuo cha mafunzo anuwai. Siero
alichagua taaluma ya uashi. Jamii nzima ilishangaa.
Iweje mtoto wa kike aingilie kazi za wanaume? Kijijini,
watu wengi waliamini kuwa msichana au mwanamke
hakustahili kufanya kazi ya uashi.
Siero alishangaa kuona kuwa hata marafiki
walioabudu pamoja walimtenga. Kwa bahati nzuri,
wazazi wake walimuunga mkono. Walimhimiza aifuate
ndoto yake.
Miaka miwili baadaye, Siero alikamilisha masomo
yake ya uashi. Hakuna aliyetaka kumpa ajira kijijini.
Waashi wa kiume walikataa kumshirikisha kazini.
Kijiji kilipomkataa, Siero alielekea mjini.Nyota ya Siero
ilianza kung’aa. Alipopata nafasi ya kwanza ya kazi, Siero
aliifanya kazi yake kwa ustadi mkubwa. Miezi michache
baadaye, sifa za Siero zilikuwa zimeenea kote mjini.
Akawa anapata kazi nyingi ajabu.
Siku moja, Siero alirudi kijijini kwa gari la kifahari.
Waliompinga, hawakuamini macho yao. Naye Siero