Page 40 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 40
9. Magonjwa
Mlango 17. Kinga ni Bora kuliko Tiba
Mlango 18. Afya Bora kuliko Mali
Kusoma
Kusoma kwa mapana
Soma matini yafuatayo.
Matini 1
Mwamko mpya
Naikumbuka likizo ya Desemba mwaka uliopita.
Nilienda kumtembelea shangazi Rukia. Shangazi alikuwa
mwanabiashara sokoni. Alikuwa na wana wawili:
msichana wa miaka minne na mvulana wa miaka mitano.
Alikuwa akituletea keki, peremende, biskuti na soda kila
jioni. Mara nyingine, alituachia asubuhi pesa za kununulia
chipsi na juisi katika kibanda kilichokuwa karibu na
kwake.
Wakoi wangu walifurahia maisha hayo lakini mimi
sikuyafurahia. Shangazi hakuwa akienda kazini siku za
wikendi. Sote tuliandamana na shangazi hadi mtoni
Jumamosi moja. Alikuwa amebeba tita la nguo. Alizifulia
nguo hizo mtoni. Majirani wake pia walikuwa wakizifulia
nguo mtoni.
Shangazi alizianika nguo kando ya mto ili zikauke.
Zilipokauka, tulimsaidia kuzianua kisha tukavijaza vibuyu