Page 48 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 48

alikuwa ameamua kupambana na itikadi zile za
               kumbagua mtoto wa kike. Alianzisha mradi wa kujenga
               madarasa mawili katika shule ya msingi alikosomea.

               Aliwashirikisha wasichana wengine waashi kuyajenga
               madarasa yale. Baada ya madarasa hayo kukamilika,
               Siero aliandaa hafla ya kuyapokeza kwa jamii ya shule na
               wanakijiji ili yaanze kutumika.
                   Wakati wa hafla hiyo, Siero aliwashauri wanakijiji

               kutupilia mbali itikadi na imani ambazo zimepitwa
               na wakati. Wanakijiji hawakustahili kuelezwa zaidi.
               Walikuwa wamejionea wao wenyewe.
   43   44   45   46   47   48