Page 44 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 44
Kusoma
Kusoma kwa mapana
Matini ya kidijitali
Soma matini yafuatayo.
Matini 1
Matumaini ya Ivoni
“Miaka mitano sasa na mtoto hazungumzi! Ama
amerogwa au amelaaniwa!” Mzee Igoko alimfokea
mkewe.
“Baba Ivoni, usiseme hivyo. Ivoni alizaliwa na ulemavu
wa ubongo,” mkewe Igoko alijibu.
Mamake Ivoni alijua mapema kwamba mwana wao
alikuwa amepooza ubongo. Juhudi zake za kumtafutia
msaada wa kiafya ziligonga mwamba. Ukali wa mumewe
ulimjaza hofu. Alikuwa ameonywa dhidi ya kumtoa
nje. Mumewe alisema kwamba watu wangewacheka
wangegundua kwamba mwanao wa miaka mitano
hakuwa akizungumza. Basi maisha ya Ivoni yakawa ni
humo tu ndani ya chumba cha ndani.
Majirani hawakuwahi kumwona mtoto huyo kwa
miaka hiyo mitano ijapokuwa walisikia kilio chake kila
siku. Hakikuwa kilio kama cha watoto wengine. Hali hiyo
ndiyo iliwafanya wachukue hatua.