Page 45 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 45
Asubuhi moja, Mzee Igoko na mkewe walitokewa na
wageni; maafisa wa watoto wakifuatwa na majirani.
Wageni hawa walitaka kumwona mtoto aliyefungiwa
katika chumba cha ndani. Hiyo ndiyo siku maisha ya Ivoni
yalipata matumaini.
Maafisa wa watoto na wa afya waliwapongeza
majirani kwa kupiga ripoti. Hata hivyo, walisikitika
kwamba iliwachukua muda mrefu kufanya hivyo.
“Mkisikia jambo kama hili tena, chukueni hatua mara
moja ili kuwaokoa mapema watoto kama hawa,” afisa
mmoja wa watoto aliwaambia majirani.
Katika siku kadhaa zilizofuata, maafisa wa watoto na
wa afya walihakikisha kwamba Mzee Igoko na wazazi
wengine kama yeye wameelewa kwamba ulemavu
wanaozaliwa nao watoto hausababishwi na laana wala
uchawi. Ulemavu huo hutokana na matatizo ya kiafya
yanayofaa kushughulikiwa na wataalamu wa afya ya
watoto.
Matini 2
Dhehebu la ajabu
Kila mkazi wa kijiji cha Petu alimjua Mzee Kosi. Mzee
Kosi alikuwa na mke na watoto wanne. Kwa miaka mingi,
alikuwa muumini wa dhehebu moja pale kijijini. Hata
hivyo, alilihama dhehebu hilo na kujiunga na dhehebu
tofauti karibu na mji wa Kuseko.