Page 36 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 36
6. Hupendelea kutembea kutoka nyumbani hadi shuleni.
7. Mimi hupanda mimea na kuinyunyizia maji.
8. Mimi huwasaidia wazazi wangu kupambanua taka
kwani kila aina inaweza kutumiwa kwa namna tofauti.
Kwa mfano, baadhi ya taka zinaweza kutumiwa
kama mbolea, nyingine zinaweza kulishwa mifugo na
nyingine zinaweza kutengenezwa upya kwa mfano,
chupa za plastiki.
Ukipata nafasi, nawe nieleze mambo unayoyafanya huko
kijijini.
Wasalimie wote.
Mwenzako,
Titokawa.
Kuandika
Insha ya maelezo
Kielelezo cha insha ya maelezo
MITI NI UHAI
Miti ina faida chungu nzima. Bila miti, sidhani
kungekuwa na maisha ya watu na wanyama. Ukweli ni
kuwa, miti ni uhai.
Miti huvuta mvua. Majani ya miti huchangia kutungika
kwa mawingu ya mvua. Ukataji miti unaweza kuchangia
kuadimika kwa miti kama maziwa ya kuku.
Isitoshe, miti huzuia mmomonyoko wa udongo. Mizizi
ya miti hushikilia udongo ili usibebwe na maji na upepo.
Mbali na hayo, majani ya miti hukinga udongo hutokana
na kupigwa moja kwa moja na matone ya mvua. Miti
pia hupunguza kasi ya upepo jambo ambalo pia huzuia
mmomonyoko wa udongo.