Page 35 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 35
Tulipakiwa ndani ya lori siku moja na kusafirishwa
hadi kiwandani. Humo, tulikatwakatwa zaidi. Tulioshwa
kisha tukayeyushwa na kutengenezwa upya. Wengine
wetu tulitumiwa kutengeneza fulana. Wengine
tukatengenezewa chupa zingine. Wapo waliotengenezewa
mifuko ya kulalia. Vifuniko vyetu vilitengenezewa
miswaki.
Bado niko dukani mwa kuuzia nguo nikisubiri
kununuliwa. Sijui nitafikishwa wapi. Hata hivyo,
natekeleza wajibu wangu wa kujenga taifa.
Mkiwa wawiwawili, fanyeni shughuli hizi.
1. Je, wewe hutupa wapi chupa za plastiki unazozitumia?
Mweleze mwenzako.
2. Je, wewe hutumiaje chupa za plastiki baada ya
kuzitumia? Mweleze mwenzako.
Matini 3
Kutoka kwa: titokawa@gmail.com
Mada: Naipenda dunia
Mpendwa Wematenda,
Unaendeleaje?
Ninakuandikia kukujuza kuwa yapo mambo kadhaa
ambayo mimi huyafanya ili dunia iwe bora. Mambo haya
ni kama yafuatavyo.
1. Mimi huzima taa za stima nikitoka chumbani na
nikienda kulala.
2. Mimi huepuka kutumia maji visivyo.
3. Mimi huzitupa taka kwenye biwi wala sizitupi
ovyoovyo.
4. Mimi huwalisha ndege ambao huishi karibu na
nyumba yetu.
5. Mimi hutumia pande mbili za karatasi ninapochora au
kuandika.