Page 31 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 31
na ndiyo maana walichelewa kurudi darasani. Mwalimu
aliwapa siku tatu ili wajitayarishe kwa tathmini yao
maalum.
Baada ya siku tatu, mwalimu aliwapa tathmini. Kila
mwanafunzi alielekezwa asiketi karibu na mwenzake
darasani. Kila mmoja alipokezwa karatasi ya tathmini.
Kila mmoja aliisoma.
1. Jina . (alama 1)
2. Je, ni gurudumu lipi la gari lililopata panchari?
(alama 99)
A. La mbele, upande wa kulia
B. La mbele, upande wa kushoto
C. La nyumba, upande wa kulia
D. La nyuma, upande wa kushoto
Mkiwa wawiliwawili, fanyeni shughuli hizi.
1. Je, mnafikiri wanafunzi hao walipata alama ngapi?
Jadilianeni.
2. Umejifunza nini kutokana na kisa hiki? Mweleze
mwenzako.