Page 33 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 33
Nyuki nao walifika. Walimwambia kuwa walinuia
kufanya makao yao hapo. Baadaye, twiga walifika na
kumwomba Mzee Saka asiukate mti huo kwa sababu
walitegemea majani yake kwa chakula.
Mwanawe Mzee Saka alifika na kumwomba asiukate
mti huo kwa kuwa mara, kwa mara, ulitoa maua ya
kupendeza. Mkewe Mzee Saka alifika pia. Alimwomba
mumewe asiukate mti huo kwa kuwa aliyatumia kama
kuni matawi yake yalipokauka na kuanguka.
Jirani wa Mzee Saka alifika na kumkumbusha kuwa,
mara nyingi, waliketi kivulini mwa mti huo na kupiga
soga. Kwa nini aukate? Jirani mwingine alifika na
kumkumbusha Mzee Saka kwamba alipokuwa mgonjwa,
alimchemshia majani ya mti huo na kuyatumia maji hayo
kama dawa. Pia alimkumbusha kuwa aliweza kukata
matawi ya mti huo na kuyatumia kutengeneza nyumba
yake.
Mzee Saka alizinduka kutoka usingizini. Alishangazwa
na ndoto yake. Uchovu ulikuwa umeisha. Hewa ya hapo
chini ya mti ilikuwa safi. Ilipendeza ajabu. Mzee Saka
aliokota vifaa vyake na kurudi nyumbani. Baadaye, alirudi
na mbolea na kuitandaza shinani mwa mti huo.
Fanyeni shughuli hizi katika vikundi.
1. Kwa zamu, simulianeni kisa mlichokisoma kwa ufupi.
2. Mmejifunza nini kutokana na kisa mlichokisoma.
Elezeaneni.
3. Tambueni faida za miti zinazojitokeza katika kisa hiki.