Page 32 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 32
7. Elimu ya Mazingira
Mlango 13. Kosa Langu Mjini
Mlango 14. Mkulima Darasani
Kusoma
Kusoma kwa mapana
Soma matini yafuatayo.
Matini 1
Ndoto ya Mzee Saka
Hapo zamani, aliishi mzee mmoja aliyeitwa Saka.
Nyumba ya mzee huyo ilikuwa karibu na msitu. Siku moja,
alichukua shoka na upanga na kuelekea msituni. Alinuia
kuukata mti mmoja uliokuwa karibu na nyumba yake.
Alianza kuukata mti shinani. Mti huo ulikuwa na
shina pana. Aliendelea kukata hadi akachoka. Aliketi
kupumzika. Kutokana na uchovu, alishikwa na usingizi
mzito. Alipokuwa usingizini, aliota ndoto ya ajabu. Ndege
walikuwa wakija sikioni mwake. Walimwomba asiukate
mti huo kwa kuwa walijenga viota vyao kwenye matawi
yake. Nyani nao walikuja wakamlilia asiendelee kuukata
mti huo. Walimwambia kuwa waliishi kwenye mti huo na
hata kula matunda yake.