Page 34 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 34
Matini 2
Maisha yangu kama chupa ya plastiki
Tulitengenezewa kiwandani; mimi na ndugu zangu.
Ndugu zangu walichukuliwa na kutiwa juisi. Wengine
walitiwa soda. Mimi nilitiwa maji safi ya kunywa.
Nilibebwa na kupelekwa hadi dukani. Nilikaa dukani kwa
siku chache. Nilinunuliwa na mteja mmoja siku moja.
Punde, alinifungua na kuyanywa maji yote.
Nilidhani angenitupa kwenye biwi la taka. Hakufanya
hivyo. Alinibeba hadi kwake nyumbani. Alinitia maji
mengine aliyoyanyunyizia maua yake.
Siku moja, kulikuwa na sherehe nyumbani kwa mtu
huyo. Mtu huyo alikata maua na kuyaweka mdomoni
mwangu na kuipamba meza yake. Sherehe zilipoisha,
aliyatupa maua yale. Watoto wake walinichukua na
kunikata vipande viwili. Nusu ya chini walinitia mchanga
na kunipandia mmea. Nusu ya juu walinitengeneza na
kuzipanga kalamu zao ndani yangu.
Baada ya miezi michache, mmea uliondolewa na
kupandwa shambani. Nami nilitupwa jaani. Hata sehemu
yangu iliyokuwa ikiwekwa kalamu ilitupwa pia. Mtu
mmoja aliyebeba gunia aliniokota. Alinipeleka katika stoo
yake. Tulikuwa wengi humo. Tulikuwa tumekatwakatwa,
kupondwa na kuchafuliwa.