Page 29 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 29
“Yeye atasafiri hadi kituo cha mwisho cha garimoshi.”
“Safari yangu haitaishia hapo,” mzee alisema.
“Unasafiri hadi wapi?” Mwuzatiketi alimwuliza.
“Je, ni nani atanitetea siku ya kiama mbele ya
Muumba kwa kosa la kutolipia kifurushi changu? Hili
ni garimoshi la umma na kila mtu anastahili kufuata
sheria na kulipa nauli inayofaa bila mapendeleo.” Mzee
alimwambia mwuzatiketi huku akimpa pesa za tiketi ya
kifurushi.
Mkiwa wawiliwawili, fanyeni shughuli hizi.
1. Je, ungekuwa mzee huyo, ungefanya nini? Mweleze
mwenzako.
2. Mwambie mwenzako umejifunza nini kutokana na
hadithi hii.
Matini 3
Fadhila za punda
Zamani sana, aliishi mfanyabiashara mmoja. Alifanya
biashara ya kununua na kuuza chumvi. Alimtumia punda
wake kubeba chumvi hiyo. Alimtunza vizuri. Kumbe
fadhila za punda huyo zilikuwa mashuzi!
Siku moja, punda huyo alipokuwa na mzigo wa chumvi
mgongoni, aliteleza na kuanguka mtoni. Mwanabiashara
alifanya haraka na kumtoa punda wake mtoni.
Punda aligundua mzigo wake ulikuwa mwepesi.
Alifurahi sana. Chumvi nyingi ilikuwa imeyeyuka majini.