Page 28 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 28

“Hili si langu,” Mtema alisema.

                   “ Huoni ni la dhahabu na lina thamani kubwa?”
               Malaika alimuuliza.
                   “Naam, lina thamani kubwa lakini langu ni la chuma,”
               Mtema alijibu.

                   Malaika alitabasamu na kulitoa shoka la chuma
               majini. Mtema alilitambua shoka lake mara moja.
               Alimshukuru Malaika.
                   Malaika alimpa Mtema yale mashoka ya fedha na

               dhahabu. Mtema alimshukuru Malaika zaidi.

               Matini 2
                                 Mwuzatiketi na mzee mwadilifu



















                   Siku moja, mzee mmoja alifika katika kituo cha
               magarimoshi. Alitaka kusafiri. Alibeba kifurushi kikubwa.
               Alipofika kwenye kituo cha garimoshi, aligundua kuwa

               mwuzatiketi alikuwa jirani yake. Mwuzatiketi alimwambia
               mzee huyo alipe nauli tu wala asikilipie kifurushi.
                   “Nitakuwa katika garimoshi hilo kwa hivyo hakuna
               mtu atakusumbua kwa kukosa kukilipia kifurushi,”
               mwuzatiketi alimwambia mzee.

                    “Je, ukifika kituoni na ushuke nani atanisaidia katika
               sehemu hiyo nyingine ya safari?” Mzee alimwuliza.
                   “Usiwe na wasiwasi, nitakuacha mikononi mwa
               mwenzangu.”

                   “Mwenzako huyo atasafiri hadi wapi?” Mzee aliuliza.
   23   24   25   26   27   28   29   30   31   32   33