Page 27 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 27
Kusoma
Kusoma kwa mapana: matini
Soma matini yafuatayo.
Matini 1
Kisa cha Mtema na Malaika
Hapo zamani aliishi mtemakuni aliyeitwa Mtema.
Mtema alitumia shoka lake kupasua magogo ya kuni.
Alijipatia riziki kwa kazi hii. Licha ya kazi yake, Mtema
aliwahimiza wanakijiji wenzake kupanda miti kwa wingi.
Hata yeye alipanda miti mingi kila msimu wa mvua.
Siku moja alikuwa akipasua gogo kando ya mto. Shoka
lake la chuma lilichomoka kutoka kwenye mpini wake
na kutumbukia mtoni. Mtema alilitafuta bila mafanikio.
Alimwomba Mola ili amsaidie.
Ghafla bin vuu, Malaika alitokea.
“Je, unatafuta nini ndugu?” Malaika alimwuliza
Mtema.
“Natafuta shoka langu. Limetumbukia mtoni kwa
bahati mbaya,” Mtema alimjibu.
Malaika alitumbukiza mkono mtoni na kutoa shoka la
fedha na kumpa Mtema.
“Shoka hili si langu,” Mtema alisema.
Malaika alilirudisha majini shoka hilo na kutoa majini
shoka la dhahabu.
“Pokea shoka lako,” alimwambia Mtema.