Page 26 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 26
Sarufi
Umoja na wingi wa nomino katika ngeli ya U-YA
Sikiliza nomino za ngeli ya U-YA zikisomwa.
Umoja Wingi
1. ugonjwa magonjwa
2. upishi mapishi
3. unyoya manyoya
4. ulezi malezi
5. ubua mabua
6. ubele mabele
7. utete matete
8. ulio malio
Umoja na wingi wa sentensi katika ngeli ya U-YA
Sikiliza sentensi zenye nomino za ngeli ya U-YA zikisomwa.
1. Umoja. Ugonjwa uliozuka umedhibitiwa.
Wingi. Magonjwa yaliyozuka yamedhibitiwa.
2. Umoja. Ulezi wake unazingatia nidhamu.
Wingi. Malezi yao yanazingatia nidhamu.
3. Umoja. Ubua utalishwa ng’ombe.
Wingi. Mabua yatalishwa ng’ombe.
4. Umoja. Ulio safi umetiwa chakula.
Wingi. Malio safi yametiwa vyakula.
5. Umoja. Upishi huo unazingatia lishe bora.
Wingi. Mapishi hayo yanazingatia lishe bora.