Page 25 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 25
Na uhuni ukakoma, hekima wakathamini,
Ikaingia neema, pembe zote kijijini,
Hakika wakaungama, watailinda amani,
Na maadili daima, wakatia maanani.
Shairi 2
Maadili niyaghani
Sikio nitegeeni,
Shairi nikaririni,
Maadili niyaghani.
Amani idumisheni,
Haki zizingatieni,
Na heshima mthamini.
Uadilifu chungeni,
Umoja kumbatieni,
Na upendo upendeni.
Usawa hakikisheni,
Wajibu utimizeni,
Na uzalendo lindeni.