Page 23 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 23
Sarufi
Umoja na wingi wa nomino katika ngeli ya U-ZI
Sikiliza nomino za ngeli ya U-ZI zikisomwa.
Umoja Wingi
1. wimbo nyimbo
2. wakati nyakati
3. ufagio fagio
4. ukuta kuta
5. ufa nyufa
6. ulimi ndimi
7. ufizi fizi
8. umbavu mbavu
9. wembe nyembe
10. waraka nyaraka
Umoja na wingi wa sentensi katika ngeli ya U-ZI
Sikiliza sentensi zenye nomino za ngeli ya U-ZI zikisomwa.
1. Umoja. Wimbo unasikika vizuri.
Wingi. Nyimbo zinasikika vizuri.
2. Umoja. Wembe unaotumika ni safi na salama.
Wingi. Nyembe zinazotumika ni safi na salama.
3. Umoja. Ufa utazibwa mapema.
Wingi. Nyufa zitazibwa mapema.
4. Umoja. Ukurasa wote unasomeka kwa urahisi.
Wingi. Kurasa zote zinasomeka kwa urahisi.
5. Umoja. Ukwato wa ng’ombe umetibiwa.
Wingi. Kwato za ng’ombe zimetibiwa.