Page 22 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 22

Shairi 2

                                         Ukata hauna tamu

































                   Sio wema ufukara, kwa yeyote mwanadamu,

                   Huleta mengi madhara, maisha kuwa magumu,
                   Bila kujali majira, ufukara huhujumu,

                   Ufukara sio bora, usikubali udumu.

                   Usikubali udumu, ipende yako elimu,

                   Masomo uyaheshimu, uepuke hali ngumu,
                   Kamwe usikudhulumu, ufukara uhukumu,

                   Ukata hauna tamu, wala haunayo hamu.

                   Wala haunayo hamu, na usiupe sehemu,
                   Hakika na ufahamu, yako kazi iheshimu,
                   Hata kazi iwe ngumu, itakupa darahimu,

                   Ukipata darahimu, zitumie kwa nidhamu.
   17   18   19   20   21   22   23   24   25   26   27