Page 21 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 21

Kusoma kwa ufahamu


               Shairi 1
                                         Fimbo ya umaskini



































                   Hapo kale aliishi, bibi mmoja maskini,
                   Hangeweza na mapishi, kupika kwake nyumbani,

                   Zake nguo si ucheshi, zilikuwa mashakani,
                   Yake afya si ubishi, ilikuwa taabani.

                   Uamuzi alitoa, kumaliza umaskini,
                   Umilisi akajua, ni fimbo ya umaskini,

                   Vitabu akabukua, ujuzi akabaini,
                   Na mbinu akagundua, mapato yake kubuni.

                   Uhitaji ukamwisha, nyumba njema akajenga,

                   Akawa na mlo tosha, maradhi akakinga,
                   Nguo akabadilisha, zile mbovu akatenga,
                   Maisha akanyoosha, na vitabu hakufunga.
   16   17   18   19   20   21   22   23   24   25   26