Page 18 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 18
Umoja na wingi wa sentensi katika ngeli ya I-ZI
Sikiliza sentensi zenye nomino za ngeli ya I-ZI zikisomwa
kwa kifaa cha kidijitali.
1. Umoja. Sabuni inayotumiwa kunawa inanukia.
Wingi. Sabuni zinazotumiwa kunawa zinanukia.
2. Umoja. Saa iliyonunuliwa ilipendeza.
Wingi. Saa zilizonunuliwa zilipendeza.
3. Umoja. Siku iliyongojewa imewadia.
Wingi. Siku zilizongojewa zimewadia.
4. Umoja. Sahani itakayotumika, itaoshwa vizuri kwa
sabuni.
Wingi. Sahani zitakazotumika, zitaoshwa vizuri kwa
sabuni.
5. Umoja. Nyumba inayojengwa inapendeza.
Wingi. Nyumba zinazojengwa zinapendeza.