Page 17 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 17
Mkiwa wawiliwawili, fanyeni shughuli zifuatazo.
1. Msimulie mwenzako kisa ulichokisoma kwa ufupi.
2. Umejifunza nini kutokana na kisa ulichokisoma?
3. Tambueni msamiati mpya kwenye kifungu na uutafutie
maana.
4. Jitahidi kuutumia msamiati huo katika mazungumzo
yako ya kila siku.
Sarufi
Umoja na wingi wa nomino katika ngeli ya I-ZI
Sikiliza nomino za ngeli ya I-ZI zikisomwa.
Umoja Wingi
1. saa saa
2. siku siku
3. sahani sahani
4. sabuni sabuni
5. kalamu kalamu
6. karatasi karatasi
7. nyumba nyumba
8. simu simu
9. nguo nguo
10. glovu glovu
11. sindano sindano
12. dawa dawa
13. sauti sauti
14. chati chati
15. chupa chupa