Page 16 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 16
Kifungu 4
Soma kifungu kifuatacho.
Siku ya mazingira
Niliamka saa thenashara macheo. Nilijitayarisha kwa
muda wa saa moja hivi. Mwendo wa saa moja na dakika
kumi asubuhi, nilianza safari kuelekea eneo ambalo
lililopangiwa kupandwa miti.
Tulifika huko saa moja na nusu asubuhi. Watu
wachache walikuwa wamefika. Tuliwangoja watu zaidi
wafike. Baadaye, tulitembea hadi karibu na Mto Rui
uliokuwa uwekauka. Chifu na wanamazingira wengine
wangepanda miti kando ya Mto Rui siku hiyo.
Tulifika mtoni saa tatu kasoro robo. Tayari chifu na
watu wengine walikuwa wamefika. Mara moja, shughuli
zilianza. Sisi hatukupanda miti ila tuliwasaidia tu watu
wazima kwa shughuli ndogondogo.
Shughuli hizo ziliendelea hadi saa nane alasiri.
Baada ya hotuba fupi ya chifu, kila mtu aliondoka. Watu
wazima walituongoza hadi sokoni. Tulifika sokoni saa
tisa alasiri. Tulinunuliwa vyakula na matunda. Baadaye,
tuliandamana nao hadi nyumbani.
Tuliagana na kila mtu akaelekea nyumbani. Nilifika
nyumbani magharibi. Nilioga na kupumzika. Thenashara
machweo, nilikula kilalio changu. Baadaye, nilienda
kulala.