Page 13 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 13
majilisini. Alibaki hapo hadi saa sita adhuhuri kisha
mwalimu akamsindikiza hadi kwenye lango la shule.
Kifungu 2
Soma matini yafuatayo.
Funzo la Fuai
Fuai alialikwa na Babu Leposo kwa safari. Alifurahi
kwa sababu alikuwa ameanza likizo. Wawili hawa
wangeondoka kwa garimoshi la saa mbili na dakika kumi
asubuhi ya siku iliyofuata. Kituo cha garimoshi hakikuwa
mbali na nyumbani kwao.
“Mimi nitaondoka nyumbani saa moja na robo ili
nisichelewe,” Babu Leposo alimwambia Fuai.
Siku ya safari, Fuai aliamka alfajiri. Alitazama saa na
kuona ilikuwa saa kumi kamili. Alirudi kulala.
Baadaye, aliamka saa mbili kasoro dakika ishirini
asubuhi. Alijitayarisha chapuchapu. Alifika katika kituo
cha garimoshi saa mbili na dakika tisa. Milango ya
garimoshi ilikuwa tayari imefungwa. Garimoshi lililiza
king’ora cha kuondoka. Fuai alilikodolea macho garimoshi
huku likiondoka. Alijawa na fedheha.
Babu Leposo alirudi nyumbani jioni ya siku hiyo. Fuai
alinuna alipomuona.
“Mbona hungeningoja kwa dakika moja tu?” Fuai
alimwuliza babu yake.