Page 15 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 15

Ghafla, alinaswa mguu. Alipoangalia, aliona ni mtego.
               Lo! Alikuwa amenaswa na mtego alioutega Mzee Kiomo.
               Aliutega mtego huo ili kunasa wanyama waliopitia njia

               hiyo na kuharibu mimea na wengine kula kuku wake.
               Mbweha alijaribu kujinasua lakini akashindwa.
                   Saa sita adhuhuri, Mzee Kiomo alifika na kumwona
               Mbweha. Mbweha alijitetea. Mzee Kiomo aliondoka
               na kumwacha Mbweha hapo. Alirudi saa nane alasiri.

               Mbweha alitarajia kupokea adhabu kali lakini Mzee
               Kiomo alimnasua na kumwacha aende zake.
                   Mbweha alitimua mbio hadi shereheni. Hakumpata
               yeyote huko. Aliketi na kulia kwa muda mrefu. Baadaye,
               aliondoka kuelekea kwake. Alifika kwake saa thenashara
               jioni. Alijuta sana kwa makosa yake.

               Fanya shughuli zifuatazo.
               1.   Msimulie mwenzako kifungu hiki kwa ufupi.

               2.   Umejifunza nini kutokana na kifungu hiki?
               3.   Unafikiri ni makosa gani Mbweha aliyafanya?

               4.   Tambua msamiati mpya kwenye kifungu na uutafutie
                   maana.
               5.   Jitahidi kuutumia msamiati huo katika mazungumzo
                   yako ya kila siku.
   10   11   12   13   14   15   16   17   18   19   20