Page 12 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 12
Kusoma
Kusoma kwa mapana: matini ya kidijitali
Kifungu 1
Soma kifungu kifuatacho.
Mgeni darasani
Asubuhi hiyo ya Ijumaa ilikuwa ya kipekee kwetu.
Tulimtarajia mgeni katika darasa letu. Kufikia saa nne
kasoro dakika ishirini, tulikuwa tumetulia darasani tayari
kumpokea mgeni wetu.
Mgeni alifika saa nne kamili asubuhi. Sote tulisimama
na kumkaribisha. Alituelezea mengi kuhusu hatua
za kiusalama wakati wa kutumia vifaa vya kidijitali.
Alitushauri kila wakati tuyasome matini kutoka tovuti
salama tu. Alituonya kuwapa watu tusiowajua habari za
kibinafsi mtandaoni. Habari hizo za kibinafsi ni kama vile:
majina yetu, majina ya wazazi na walezi wetu na nambari
zao za simu.
Mgeni alitushauri tusiwasiliane na watu tusiowajua
mtandaoni. Mbali na hayo, alitusihi tusifungue tovuti
ambazo hatuna uhakika kuzihusu. Aidha, tukiona jambo
lolote mtandaoni ambalo linatutia wasiwasi, tufunge
tovuti husika. Vilevile, turipoti jambo hilo kwa mwalimu,
mzazi, mlezi au mtu mwingine mwenye uwajibikaji.
Mgeni wetu alimaliza mazungumzo yake saa tano
na nusu. Tulimshukuru kwa ushauri wake. Tulimwahidi
kwamba tungezingatia ushauri huo. Tulimuaga
akaondoka. Aliandamana na mwalimu wetu hadi