Page 6 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 6
11. Thuluthi ya dhahabu yenye thamani kubwa ilinunuliwa
na wateja thelathini waliodhamiria kuitumia kama
dhamana ya kukopa fedha katika benki.
Kusoma
Msamiati wa mapishi
1. Njia mbalimbali za kupika
a) kukaanga
b) kuchemsha
c) kuchoma
d) kuoka
2. Aina za vyakula
a) ugali au sima
b) pure
c) wali
d) biriani
e) pilau
f) matoke
g) kima
h) viazi vitamu
i) viazi vikuu
j) viazi wanga
k) mbatata
3. Viungo vya kupikia
Viungo huongeza ladha na harufu nzuri kwenye chakula.
a) bizari
b) nyanya
c) dania
d) mgiligilani
e) vitunguu
f) pilipili
g) chumvi