Page 5 - Kiswahili Grade 5 Yaliyomo ya kidijitali
P. 5
1. Mapishi
Mlango 1. Sherehe Kijijini
Mlango 2. Baada ya Dhiki Faraja
Kusikiliza na kuzungumza
Vitanzandimi
Sikilizeni vitanzandimi vikikaririwa.
1. Tulifurahia vuta nikuvute kati ya mafundi na wavuvi
ilipofuatwa na maafikiano badala ya vita.
2. Mvulana aliyevaa fulana aliketi kwenye fomu na
kukariri silabi za sauti f na v.
3. Sisi sote huzima taa zote za sitima tunapoondoka ili
nguvu za sitima zisitumike kiholela.
4. Mlariba huyo aliharibu sifa kwa kutoza riba ya juu.
5. Si siri siku hizi changamoto za maisha zazidi
kuongezeka kwa kasi sana.
6. Matumizi mazuri ya hela yaliimarisha ujasiriamali na
utekelezaji wa miradi tele ya serikali.
7. Askari mlinzi alivaa fulana ya rangi ya buluu na
kushika rungu kwa mkono wa kulia.
8. Walishirikiana na kuchanga takribani shilingi milioni
mbili za kukabiliana na kero lolote la uchafuzi wa
mazingira.
9. Maria alivaa rinda la rangi ya buluu na blausi ya
hudhurungi.
10. Walipotuletea redio tusikilize habari kamili, tulifanya
maamuzi haraka kabla ya robo saa kuisha wala jambo
lolote kutekelezwa.